Andiko la Maandiko: Yoshua 9:1-13:7
Mstari wa Kukariri: “Bwana akamwambia Yoshua, Usiwaogope; kwa maana nimewatia mikononi mwako; hapana mtu hata mmoja wao atakayesimama mbele yako.” Yoshua 10:8
Utangulizi:
Habari za ushindi wa kijeshi wa Israeli ziliwafanya wafalme wote wa Kanaani kuungana dhidi ya Yoshua na Israeli. Lakini wakazi wa jiji la Gibeoni walijificha wakiwa wamevaa mavazi ya zamani yaliyoraruka na viatu vilivyowekwa viraka na kumwambia Yoshua kwamba walikuwa wametoka nchi ya mbali sana. Kwa msingi huu, Waisraeli walifanya agano na Wagibeoni. Siku tatu baadaye mpango huo