Andiko la Maandiko: Waamuzi 7:1-9:57
Mstari wa Kukariri: “Bwana akamwambia Gideoni, Watu walio pamoja nawe ni wengi mno hata nisiwatie Wamidiani mikononi mwao, wasije Israeli wakajisifu juu yangu, wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa.” Waamuzi 7:2
Utangulizi:
Ili ushindi dhidi ya Midiani uweze kuwa wa kimungu, Bwana kwanza alipunguza jeshi la Gideoni kutoka 32,000 hadi elfu kumi kwa kuwarudisha nyumbani waliokuwa na woga na mioyo dhaifu, kama sheria ilivyoamuru. Jeshi hilo bado lilipunguzwa zaidi kwa kuwajaribu wanajeshi mtoni. Wale waliokunywa maji kwa njia ya kuchuruzika kama