Nitakufundisha na kukuonyesha njia unayopaswa kuifuata; Nitakuongoza kwa jicho langu. -Zaburi 32:8
Usomaji wa Maandiko: Yeremia 32:1-15
Utangulizi
Vipi kama nchi uliyokuwa ukiishi ingeshambuliwa na wanajeshi wa adui, na kundi kubwa la jeshi lao lilikuwa karibu kuteka mji mkuu? Je, kununua kipande cha ardhi karibu na mji mkuu kungeingia akilini mwako? Labda sivyo. Wengi wetu labda tungefikiria kukimbia ili kuokoa maisha yetu!
Kununua mali isiyohamishika hakungemjia Yeremia pia isipokuwa Mungu amwambie afanye hivyo. Na ndivyo alivyofanya.