Usomaji wa Maandiko: 2 Petro 1:16-21.
Mstari wa Kukariri: “Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Simba amenguruma! Ni nani asiyeogopa? Bwana Mungu amenena! Ni nani awezaye kuacha kutabiri?” (Amosi 3:7-8)
UTANGULIZI:
Dhambi ya Adamu iliwaleta wanadamu wote chini ya laana ya dhambi, kifo cha Adamu; na kama Muumba mwenye uvumilivu hangetoa njia ya kutoroka, ingekuwa kifo cha milele (Warumi 5:12; 6:23). Kwa hekima isiyo na kikomo, Mungu aliona mwisho tangu mwanzo. Baada ya kuumba vitu vyote kwa raha yake, alihuzunika alipoona